Usiku wa jana Oktoba 26, 2024 kwenye uwanja wa Santiago Bernabeu ulichezwa mchezo wa El Clasico klabu ya Real Madrid iliikaribisha klabu ya mpira wa miguu ya Barcelona katika muendelezo wa michezo ya ligi kuu nchini Hispania La liga.
Usiku wa jana Oktoba 26, 2024 kwenye uwanja wa Santiago Bernabeu ulichezwa mchezo wa El Clasico klabu ya Real Madrid iliikaribisha klabu ya mpira wa miguu ya Barcelona katika muendelezo wa michezo ya ligi kuu nchini Hispania La liga.
Barca imepata ushindi wa goli 4-0 mbele ya mahasimu wao wakubwa kitu kilichowafurahisha zaidi Mashabiki wa Barca Duniani kote ni kushinda dhidi ya Madrid kwenye uwanja wao wa nyumbani.
Kabla ya mchezo wa jana wa El Clasico kuchezwa Mabingwa watetezi wa La liga Los Brancos ilikuwa inapambania rekodi ya kucheza michezo 43 bila kupoteza rekodi ambayo ilikuwa inashikiliwa na Barcelona ya kucheza michezo 43 bila kupoteza kuanzia 2017-2018 na kuitibulia Madrid kufikia rekodi yao.
Vijana wa Kocha raia wa Ujerumani Hansi Flick walikuwa kwenye ubora mkubwa mchezo wa jana na kufanikiwa kushinda kwa ushawishi kuanzia kumiliki mchezo, kutengeneza nafasi na kuzitumia. Robert Lewandoski alifunga goli mbili huku Raphinha na Lamine Yamal wakihakikisha wanaondoka mji mkuu wa Hispania na alama zote tatu kwa kufunga mara moja kila mmoja.
Real Madrid ilizidiwa kila kitu ndani ya uwanja kuanzia kwenye mbinu mpaka mchezaji mmojammoja, Kylian Mbappe na Vinicius JR hawakuwa na siku nzuri uwanjani kwa kazi iliyofanywa na kikosi cha Wapinzani wao kucheza kwenye mfumo wa mtego wa kuotea yaani High line defending tactics ( offside traps ) wakajikuta muda mwingi mikimbio yao yote ilikamatwa kwenye mtego wa kuotea na Refarii.
Marc Casado na Pedri walikuwa kwenye ubora mkubwa jinsi walivyoamua kuifanya mechi yote ichezwe kwenye vichwa na miguu yao, walifanya kila kitu kipite kwenye himaya yao kuanzia kuiamuru Barca muda wa kukimbia na muda wa kucheza taratibu kwa kutafuta njia sahihi na rahisi za kuwafungua Wapinzani.
Maswali yameanza kuulizwa juu ya mustakabali wa Carlo Ancelotti ndani ya Real Madrid baada ya msimu wa 2024-2025 kumalizika kutokana na kiwango kinachoonyeshwa na kikosi hiko kwenye ligi na klabu bingwa Ulaya ambapo haijanza vizuri na timu imekosa uwiano sahihi kwenye kuzuia na kushambulia kama itamaliza bila kushinda kombe lolote msimu huu safari ya Muitaliano huyo ndani ya Mabingwa hao wa kihistoria wa ligi kuu nchini Hispania inaweza kufika tamati mwezi June 2026.