Kevin Durant amefunga kwenye dakika za nyongeza na kuipa ushindi timu yake ya Phoenix Suns wa Vikapu 116 dhidi ya vikapu 113 vya Los Angeles Clippers usiku wa Oktoba 23, mchezo uliochezwa uwanja wa Intuit Dome.
Kevin Durant amefunga kwenye dakika za nyongeza na kuipa ushindi timu yake ya Phoenix Suns wa Vikapu 116 dhidi ya vikapu 113 vya Los Angeles Clippers usiku wa Oktoba 23, mchezo uliochezwa uwanja wa Intuit Dome.
Mchezo huo ulikuwa wa ushindani mkubwa huku Nyota wa Los Angeles Clippers James Harden alikosa mitupo huru miwili ambayo ingefanya kuisawazishia Clippers sekunde ishirini za mwishoni mwa mchezo. Durant alimaliza mchezo akiwa amefunga alama 25 huku Harden akifunga alama 29 na ribaundi 12, Ivica Zubac yeye amefunga alama 21.
MVP huiyo wa mwaka 2014 alikuwa kwenye kiwango bora usiku wa jana na alifunga kwenye sekunde 30 za mwisho na kuufanya mchezo kumalizika sare ndani ya dakika za kawaida kabla ya kuongezwa kwa dakika na kupata ushindi kwenye muda wa nyongeza.
Durant mwenye umri wa miaka 36 alitumia uzoefu wake vizuri kwa kuihakikishia ushindi Phoenix Suns na kuifanya ianze vizuri kwenye msimu mpya wa NBA 2024-2025. Anatajwa kuwa mmoja wa Wachezaji bora wa kukapu kwenye historia ya NBA.
Nyota huyo wa zamani wa Brooklyn Nets,Oklahoma City Thunder,Seattle SuperSonics,Golden State Warriors, amekuwa na muendelezo mzuri wa kiuchezaji tangu achaguliwe kucheza ligi kuu ya kikapu nchini Marekani mwaka 2007, pamoja na kushinda ubingwa wa NBA 2 amewahi kushinda tuzo binafsi za MVP mwaka 2014, MVP wa Wachezaji nyota, Mfungaji wa pointi nyingi kwenye msimu mmoja mara 4.
Suns wamesalia California itacheza dhidi ya Los Angeles Lakers siku ya Ijumaa , wakati Clippers itasafiri kuifuata Denver Nuggets siku ya Jumamosi. Stephen Curry alifunga alama 17 na kuiwezesha Golden State Warriors kushinda kwa vikapu 139-104 dhidi ya Portland Trail Blazers kwenye muendelezo wa michezo ya ligi kuu ya kikapu nchi Marekani msimu wa 2024-2025