Thursday , 17th Oct , 2024

Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa, amewataka Watanzania kuwa na namba ya kitambulisho cha Taifa yani NIDA, ili kurahisha huduma za kidigitali zitakazomtambua kila raia kwa namba yake.

Kassim Majaliwa, Waziri Mkuu wa Tanzania

Waziri Majaliwa ameyasema hayo leo wakati anafunga kongamano la nane la TEHAMA, leo jijini Dar es Salaam, kwenye ukumbi wa kimataifa wa Mikutano wa JNICC, na kuwataka kuendana na mabadiliko ya Teknolojia Duniani
"Katika kukuza uchumi wa kidijitali nchini Serikali inakusudiwa lazima kuwepo namba ya pekeke itakayomuwakilisha raia katika kupata huduma za kiserikali na sekta binafsi ambapo namba ya NIDA ndio imechaguliwa kuwa namba ya jamii itakayorahisisha huduma na kufanya miamala katika huduma mbalimbali bila kutumia fedha taslimu badala yake itakuwa inatumika namba ya NIDA", Kassim Majaliwa, Waziri Mkuu.

Kwa upande wake Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Jerry Silaa, anasema kwa sasa wizara imeanza maandalizi ya urushaji wa Satelite.
"Wizara imeanza maandalizi ya urushaji wa Satelite ambapo mpango mkakati wa miaka mitano ya programu ya anga za juu umeanza kuandaliwa maandalizi ya utungaji wa sera, sheria, na mikataba ya kimataifa ya anga za juu unaendelea , na kwenye eneo hili tayari taasis ya teknolojia Dar es Salaam(DIT), imepata mradi wa utafiti wa kuwezesha kurusha satelite kupitiwa mradi unaosimamiwa na taaisi ya umoja wa mataifa inayosimamia maswala ya anga za juu yani United Nations ikishirikiana na taasisi ya anga za juu ya Japan", Jerry Silaa, Waziri wa HMTH.

Nae mkurugenzi Mkuu wa Tume ya TEHAMA nchini Dokta Nkundwe Mwasaga, anaelezea faida za kongamano hilo.
"Tulikuwa tunaangalia ni jinsi gani tunaweza kulichagiza hii akili unda ili kujua kwamba tunawezaje Tanzania na ikawa kitovu cha eneo hili kuweza kutengeneza  kampuni nyingi za vijana ambzo zitakuwa zinatoa huduma kwa Tanzania na nje ya Tanzania", Dkt.Nkundwe Mwasaga, Mkurugenzi Mkuu Tume ya TEHAMA.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, amesema amefurahishwa na uwepo wa kongamano hilo lililofanyika lwa lugha ya Kiswahili.
"Mimi niseme kwamba tunashukuru sana tumejifunza mambo mengi na nimefurahi sana kongamano hili limefanyika kwa lugha ya Kiswahili na mimi kama mwana kiswahili nafurahia lengo linaenda kutimia kwa sababu watu wanakuwa wameelewa zaidi", Albert Chalamila, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.