Wednesday , 9th Oct , 2024

Abraham Lincoln alikuwa mwanasiasa kutokea nchini Marekani ambaye alihudumu kama Rais wa 16 wa taifa hilo kuanzia mwaka 1861 hadi alipouawa mwaka 1865.

Haya ni baadhi ya mambo aliyopitia kwenye maisha yake, kwa upande wako ungeweza kuvaa viatu vyake?

Rais wa 16 wa Marekani, Abraham Lincoln

 

1816 : alilazimishwa kutoka nyumbani kwenda kujitegemea ili aisaidie familia yake.

 1818 : alimpoteza Mama yake akiwa na umri wa miaka 9 pekee

1828 : Dada yake alifariki

1832 : aligombea ubunge huko  Illinois kwa mara ya kwanza, na kuishia kuangukia pua 

1833 : alikopa pesa kwa rafiki yake ili afanye biashara lakini mwisho wa mwaka pesa ziliisha na biashara ikafa

1834 : alifanikiwa kugombea tena ubunge na kwa awamu hii alishinda.

1835 : Mwaka wa shangwe kwani alifanikiwa kumchumbia mchumba wake, lakini isivyo bahati mchumba wake alipoteza maisha.

1836 : aliumwa kufikia kulazwa kwa miezi 6 na ndiyo mwaka ambao alitamani kuja kuwa spika wa bunge mwisho wa siku ilishindikana.

1842 : ''Kimasomaso mwanangu msimuone'' alifanikiwa kumuoa mchumba wake Marry Todd baraka ya watoto 4, lakini ni mmoja pekee ndiye alifanikiwa kufikia ukubwa (utu uzima) wengine wote walipoteza maisha wakiwa bado wadogo.

1843 : aligombea kwenye baraza la wawakilishi lakini aliishia kukosa nafasi.

1846 : aligombea tena akafanikiwa kushinda, akahamia zake Washington

1848 : aligombea kwa mara nyingine kutetea kiti chake, bahati haikudondokea upande wake akapoteza uwakilishi.

1850 : Mtoto wake wa pili Edward kwa ufupi aliitwa Eddie alifariki akiwa na miaka 3 pekee.

1854 : aligombea useneta akaishia kudondokea pua.

1856 : aliomba uteuzi wa kuwa makamu wa Rais lakini isivyo bahati alikosa kwa sababu alipata kura chini ya 100
1858 : aligombea tena useneta alikosa kwa mara nyingine.

1860 : Kwa mara ya kwanza alifanikiwa kuchagulia kuwa Rais wa taifa la Marekani, kupitia tiketi ya chama cha Republican 

1865 : alipigwa risasi na kupoteza maisha akiwa kwenye ukumbi wa Ford's Theatre na mdunguaji aliyefahamika kwa jina la John Wilkes Booth