Tuesday , 8th Oct , 2024

Katibu mkuu chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA John Mnyika amewahimiza wananchi na wafuasi wa chama hichi kuhakikisha wanajiandikisha kwa ajili ya kupiga kura kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa na vitongoji.

Katibu mkuu wa CHADEMA John Mnyika akizungumza na wanahabari katika ofisi za makao makuu ya chama hicho mikocheni

Zoezi hilo ambalo linatarajia kufanyika octoba 11 mpaka octoba 20 mwaka huu amesisitiza kwamba chama chao kitakuwa na mawakala katika vituo vya uandikishaji ambapo amesema mawakala hao watasimamia uandikishaji kwa kile alichosema chama chao kutokuwa na Imani na baadhi ya waandikishaji watakaotumika katika mchakato huo.

“Kwa kuwa tunatambua kwamba kuna dhamira ovu ya kujaribu kuhamisha orodha hiyo haramu kwa kutumia mtandao wa kutumia mabalozi na kwa ulazima walio uweka kuwa waandikishaji ni lazima wawe watumishi wa Umma tunaelewa kwamba baadhi ya watumishi wa uma wasio waadilifu wanaweza kushawishiwa na hizo mbinu haramu sisi tutakuwa na mawakala kwenye vituo mbalimbali vya kupigia kura kwenye uandikishaji kwanzia tarehe 11 mpaka 20.” Amesema John Mnyika

Sambamba na hilo katibu mkuu wa chama hicho ameitupia lawama serikali kupitia wizara ya tamisemi kwa kutohamasisha wananchi kwenda kujiandikisha ambapo amesema kitendo hicho ni kuhalalisha nia yao ovu ya kutaka kuhujumu uchaguzi serikali za mitaaa