Monday , 7th Oct , 2024

Watoa huduma za mawasiliano nchini wametakiwa kutumia muda vizuri kukamilisha ujenzi wa Minara ya mawasiliano kwani nchi yetu ipo kwenye mapinduzi ya kidijitalil hivyo huduma hiyo ni muhimu sana.

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Jerry William Silaa

Agizo hilo limetolewa na Waziri wa Waziri wa Habari Teknolojia na Mawasiliano ya Habari, Jerry Silaa wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya TEHAMA kwa walimu wa shule za Sekondari nchini yaliyofanyika Chuo cha DIT jijini Dar es Salaam.
“Watoa huduma wa mawasiliano mkamilishe mradi huu kwa sababu hatukusudii kuwaongezea muda wa ujenzi wa minara pindi muda wa ujenzi utakapokwisha yani 13, Mei2025 hivyo nitumie fursa hii kuwataka wakandarasi wote waliopewa jukumu la kujenga minara hii wanaifanya kazi hiyo kwa ufanisi mkubwa nakuimaliza kabla muda wa mkataba kuisha na mtendaji mkuu wa mfuko yuko hapa afikishe salamu zangu”, Alisema  Jerry Silaa, Waziri wa Habari.

Mtendaji mkuu wa mfuko wa mawasiliano kwa wote pamoja na mkuu wa Taasis ya Teknolojia Dar es Salaam,  DIT wanaelezea umuhimu wa mafunzo hayo kwa walimu wa shule za Sekondari.
“Uwezo wa kutumia kikamilifua vifaa vya TEHAMA, katika kufundishia pamoja na uwezo wa kiufundi kwa ajili ya kutatua matatizo madogo madogo ya vifaa vya TEHAMA pale inapotokea kwenye maeneo yao ya shule”, Alisema Mhandisi Peter Mwasalyanda, Mkurugenzi UCSAF.
“Mafunzo haya ni mwendelezo wa jitihada za Serikali katika kuboresha mazingira ya ufundishaji DIT imejipanga vizuri kutoa mafunzo ya Tehama kwa kuwa na mataal wenye sifa, Taasis inajenda kituo cha tehama kitakachotoa watalaam wa ndani na nje ya nchi”, 

Nao baadhi ya walimu wanasema watakavyotulia elimu hiyo ya TEHAMA.
“Mafunzo haya yatatusaidia sana katika kuyekeleza majukumu yetu kwenye kufundisha hatutatumia nguvu nyingi kama ilivyokuwa awali”, alisema  Abdallahman Ngoda, Mwalimu kutok Tanga
“Yatatusaidia katika kuandaa masomo na mitihani lakini pia hatutakuwa na ulazima wa kutafuta mafundi wa vifaa vya TEHAMA tutakuwa tunatengeneza wenyewe”,alisema  Juma Msuya, Mwalimu Pugu sekondari.
“Niwape woto walimu wenzangu tusibaki na ujuzi wetu tuwaelimishe na wengine waweze kujua tutakaporudi mashuleni mwetu”, alisema Suria Juma, Mwalim kutoka Zanzinar.