Monday , 7th Oct , 2024

Mbunge wa jimbo la Arusha mjini Mrisho Gambo kwa kushirikiana na nalozi wa cjina nchini Tanzania Chen Mingjian wamegawa mitungi kwa walimu wa shule za sekondari na msingi kwa jiji la arusha ikiwa ni kutekeleza kwa vitendo kampeni ya matumizi ya nishati safi ya kupikia.

Mbunge Wa Arusha mjini mrisho gambo

Akizungumza wakati wa hafla hiyo iliyofanyika mapema hii leo Mrisho gambo amesema ofisi yake kwa kushirikiana na ubalozi umedhamiria kutoa mitungi takribani 8000 kwa walimu ili kuhakikisha walimu wanakuwa mabalozi wa matumizi ya nishati safi wanapokuwa mashuleni na kuhakikisha mifumo hiyo inafungwa mashuleni kwa ajili ya kupikia chakula kwa wanafunzi.

“Nimezungumza na madam Dkt. Chen tuweze kufunga mifumo wa gesi ya kupikia kwa shule za sekondari na tutachagua shule ya mfano kama Arusha Girls  na pia tutazungumza na wadau wengine ambao tutakwenda kuwaomba watuchangie wakiwemo wadau wa utalii na makampuni mbalimbali kila kampuni na  kila kiwanda kikichukua shule moja na tukafunga ule mfumo. niwahakikishie ndani ya muda mchache tutakuwa tumefikia shule zote” Amesema Mrisho gambo mbunge wa Arusha mjini

Aidha mkurugenzi wa kampuni ya Orxy Benoit Araman amesema kampuni ya Orxy iko tayari kushirikiana na serikali kuhakikisha wanawafikia wananchi wengi kwa kuanza na walimu ambao amewataka wawe mabalozi katika vikao vya wazazi mashuleni

“Leo tuko pamoja kuunga mkoni utekelezaji wa program ya kupika kwa nishati safi nchini Tanzania ni program ambayo itachukua miaka 10 kuwezesha upatikanaji wa nishati safi ya kupikia kwa angalau asilimia 80 ifikapo mwaka 2034. kazi ni kubwa na tunahitaji kuchangia juhudi ili kampeni hii ifanikiwe tukakuhitaji wewe profesa na walimu kuwa mabalozi wa nishati safi ya kupikia kwa kuzungumza kuhusu nishati safi kwa wanafunzi wenu na katika mikutano na wazazi hii itasaidia kwa kiasi kikubwa kukuza matumizi ya nishati safi ya kupikia.” Amesema mkurugenzi wa Orxy nchini Tanzania Benoit Araman

Sambamba na hilo walimu pia wameahidi kuwa mabalozi wa nishati safi ya kupikia na kumshukuru balozi wa china na ofisi ya mbunge kwa kuchagua kuanza walimu na watahakikisha jamii nzima inanufaika na matumizi ya nishati safi ya kupikia.

“Madam chen tunakushukuru kwa kumuunga mkono mbunge wetu Mrisho Gambo kutimiza ahadi yake kukabidhi majiko 5000 ambapo wewe ulituahidi kutupa majiko 800 na hii leo umekuja kutimiza ahadi yao, madam chen majiko utakayotupa yatatusaidia sisi walimu wa jiji la arusha kuunga mkono kampeni iliyoanzisha na raisi Dkt. Samia Suluhu Hassan ya matumizi ya nishati safi mbunge anaamini walimu wote tukitumia majiko ya gesi kampeni hii matumizi ya nishati safi itaifikia jamii kubwa kwa uraisi” Amesema mwalimu Pantaleo mwakilishi wa walimu kutoka TAPSA na TAHOSA