Kijana aliyehukumiwa miaka 30 jela
Akizungumza na EATV Mkuu wa Mashtaka wilaya ya Momba Simon Peles amesema kuwa Bahati amehukumiwa kwa kifungu cha 131 kifungu kidogo cha kwanza cha sheria ya kanuni ya adhabu marekebisho ya mwaka 2022 baada ya mahakama kuthibitisha pasi na shaka kuwa alitenda kosa hilo mnamo tarehe 9/10/2023 katika kijiji cha Chiwanda na kufikishwa Mahakamani tarehe 19/10/2023 na kufunguliwa kesi namba 201 ya mwaka 2023.
Aidha Mkuu huyo ametoa wito kwa jamii kushirikiana katika kutokomeza vitendo vya ukatili na unyanyasaji wa kingono.