Boniface Jacob, meya wa zamani wa manispaa ya Ubungo
Uamuzi huo umetolewa mapema leo Oktoba Mosi, 2024 ambapo Boniface Jacob, maarufu Boni Yai, mkazi wa Mbezi Msakuzi, Dar es Salaam, mfanyabiashara na mwanasiasa wa upinzani anakabiliwa na kesi ya uchapishaji taarifa za ongo kwenye mtandao wa kijamii aina ya X.
Hata hivyo Mahakama hiyo imepiga kalenda tena uamuzi wa maombi ya awali ya upande wa mashitaka ya kuzuia dhamana ya Boni Yai, ambao awali ilikuwa imepanga kuutoa Septemba 23 ikaahirishwa mpaka Septemba 26, ambapo pia Mahakama ilishindwa kuutoa baada ya Serikali kuomba kuwasilisha kiapo cha ziada.
Mahakama hiyo imepanga kutoa uamuzi huo wa maombi ya awali ya Serikali ya zuio la dhamana Oktoba 7, 2024 hapa wakili wa chama cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA, Peter Kibatala anafafanua zaidi.