Ten Hag amesema hayo ikiwa ni maandalizi kuelekea mchezo wao wa kwanza wa msimu kwenye michuano ya UEFA Europa League watakaocheza kesho Jumatano dhidi ya FC Twente ya nchini Uholanzi katika dimba la OLD Traford.
Ten Hag amesisitiza kuwa michezo imekuwa mingi ambapo kwa msimu uliopita walikuwa na mfululizo wa michezo 87 ambapo kulikuwa na wastani wa tofauti ya masaa 67.3 kutoka mchezo mmoja hadi mchezo mwingine. Licha ya ratiba kuwa ngumu kocha huyo amesema anataka kufanya vizuri kwenye Europa League ili apate tiketi ya kucheza Ligi ya mabingwa msimu ujao wa 2025-26.