Dkt. Philip Isdor Mpango , Makamu wa Rais Tanzania
Dokta Mpango ametoa agizo hilo wakati anazindua kituo cha upandikizaji mimba pamoja na kuwasha vifaa vya kusaidia kusikia kwa viziwi kwenye Hospitali ya Taifa Muhimbili leo jijini Dar es Salaam.
“Maombi au mapendekezo ya msamaha wa kodi kwenye vifaa muhimu katika huduma za upandikizaji mimba ili kusaidia kushusha gharama kama za huduma hiyo, kwahiyo mheshimiwa Waziri wa Afya, ninakutaka ukutane sasa na waziri wa Fedha muone namna bora ya kutekeleza pendekezo hili naamini ni jambo muhimu sana”, alisema Dkt.Philip Mpango , Makamu wa Rais Tanzania.
Waziri wa Afya Jenista Mhagama amesema wizara imeandaa mfumo utakaosomana klatika Hospitali zote nchini ili kupunguza gharama za matibabu.
“Tunataka kutengeneza mifumo inayosomana, mifumo itakayopunguza gharama za matibabu na tiba nchini, sasa hivi mgonjwa anaweza akatibiwa Ruvuma Hospitali ya Mkoa, akapata vipimo, lakini akija kwenye Hospitali ya Taifa, anaanza upya vipimo kwa sababu miumo haisomani na hiyo imekuwa ikiongeza sana gharama za wananchi katika kupata huduma za matibabu, Ndani ya Wizara ya Afya tumejiwekea malengo itakapofika Mwezi wa 10/15 Hospitali zetu zote kuanzia ngazi ya chini mpaka Taifa isomane ili iwe ni suluhu ya”, alisema Jenista Mhagama, Waziri wa Afya.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila ameitaka wizara ya Afya kuweka mifumo imara ili kuzuia matapeli ambao watataka kufungua huduma hiyo baada ya kuona mahitaji makubwa ya wananchi.
“Kwakuwa jambo hili tatizo kubwa ina maana wahitaji watakuwa ni wengi, kwahiyo wanaweza wakajitokeza wengine, nimuombe waziri kuwe na udhibiti wa watoa huduma wasije wakaingia wajanja wajanja na kuifanya huduma hii chini ya kiwango”, alisema Albert Chalamila, Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Profesa Mohamed Janabi anasema 30% ya wagonjwa wanawake wanaofika Hospitalini hapo wana changamoto ya uzazi ndio maana wakaamua kuleta huduma hiyo ya upandikizaji wa mimba.
“Tuliona familia kushindwa kupata watoto, 35% yanatoka kwa akina baba na 65% kwa akina mama, tunajua ni tatizo Kila wagonjwa 10, 3/4 wana tatizo 30% wana tatizo la kupata mtoto dunia 17% Lilikuwa linapelekea migogoro Kupitia mapato ya ndani tukanunua vifaa vya Bilionin1.1, Ukarabati mil300, Upandikizaji mimba,Utunzaji wa mayai, Mayai kwa zaidi ya miaka 30 tunaweza Kwa wanaojiendeleza kwa masomo kama hawapo kupata watoto kwa sasa Kuna wataalam 10 Wakina mama 10 wapo wanafanya clinic kwa ajil ya upandikizaji”, alisema Prof. Mohamed Janabi, Mkurugenzi Hospitali ya Taifa Muhimbili .
Nae Mganga Mfawidhi Hospitali ya Rufaa mkoa wa Temeke, Dkt. Joseph Kimaro anasema huduma hiyo itasaidia wanawake ambao walikuwa wanafik Temeke wakiwa na shida hiyo na kuanzia sasa atawapatia rufaa kwenda Muhimbili.
“Huduma hii itasaidia sana pale Temeke Hospitali tumekuwa tukipokea wagonjwa wengi wenye changamoto ya uzazi kwahiyo huduma hii itasaidia sana na sisi Temeke Hospitali tutaleta wagonjwa wetu waje kupata huduma hii ya upandikizaji”, alisema Dkt. Joseph Kimaro, Mganga Mfawidhi Hospitali ya Rufaa mkoa wa Temeke.