Friday , 23rd Aug , 2024

Klabu ya Gofu ya Lugalo imejipanga vyema kufanya maandalizi kabambe kuelekea shindano la Mkuu wa Majeshi (CDF) yanayotaraji kufanyika kuanzia Oktoba 04 mpaka 6-2024.

Akizungumza na EATV,Afisa Habari wa klabu ya Gofu ya Lugalo Meja Seleman Semunyu amesema wamejipanga kufanya shindano lenye kiwango kikubwa huku kukiwa na maboresho makubwa ya zawadi kwa ajili ya kuelekea kuadhimisha miaka 60 ya Jeshi la Wananchi la Tanzania (JWTZ).

 "Lugalo Golf Club kutakuwa na mashindano ya kombe la mkuu wa majeshi CDF TROPHY 2024. yatafanyika kwa siku 3, tarehe 4,5 na 6 mwezi wa  10,2024,Mashindano yana zawadi kubwa na yamebeba dhamira ya kuenzi miaka 60 ya jeshi hili"

Kwa upande mwingine,wachezaji wa klabu ya Gofu Lugalo wameeleza maandalizi pamoja na dhamira zao kuelekea mashindano hayo huku wametamba kubeba vikombe kwenye shindano la CDF trophy 2024.
 "Timu pinzani zimejandaa vizuri ila tutahakikisha kombe linabaki nyumbani kwenye mashindano haya ya CDF 2024".