Sandungu la kupigia kura
Yamesemwa hayo na mkurugenzi mtendaji wa Foundation for civil society, Justive Rutenge wakati anaongea na wanahabari kuelekea wiki ya Azaki za kiraia.
“Tupo kwenye kipindi muhimu cha Demokrasia na mwaka huu tuna uchaguzi na mwakani tuna uchaguzi, kwahiyo ushiriki wa wananchi ni muhimu hasa katika Dira ya Taifa, ambayo imebeba maendeleo ya nchi yetu”, alisema Justice Rutenge, Mkurugenzi Mtendaji (FCS).
“Lengo ni kuhakikisha kunakuwa na ownership ili maendeleo ya nchi yetu yajengwe na watanzania wenyewe na kwenye wiki ya Azaki tutatoa Elimu kwa ajili ya ushiriki wa wananchi katika Dira ya nchi yetu”, alisema Nesia Mahenge, Mkurugenzi Mkazi CBM International.
Nao wananchi wanaelezea walivyojipanga kushiriki katika chaguzo zijazo.
“Nimejiandaa kushiriki kikamilifu sana ili niweze kupata kiongozi aliye bora anayeweza kutetea maslahi ya wananchi”, alisema Frank Juma, Mkazi wa Dar es Salaam.
“Nimeshajiandikisha kwenye daftari la wapiga kura nasubiri tu niweze kucjagua kiongozi ambae atatoa sera ambazo zitanivutia”, alisema Godfrey Robert, Mkazi wa Dar es Salaam.
“Nitachagua kiongozi ambaye anaweza kutoa fursa kwa vijana kwa sababu wengi tumesoma tupo mtaani hatuna ajira wala connection yeyote kwahiyo atakayetupa kipaumbele vijana ndiye nitamchagua”,alisema Charles Pascal, Mkazi wa Dar es Salaam.