(Timu ya Boston Celtics ikishangilia ubingwa wa NBA 2023-24)
Msimu wa NBA wa 2024-25 utashuhidia michezo miwili ya kufungua pazia ambapo bingwa mtetezi Boston Celtics aliyeshinda msimu uliopita ambaye mwenye mataji 18 akianza kampeni ya kusaka ubingwa wa 19 kwa kupambana na New York Knicks kwa upande wa Mashariki
Kanda ya Magharib itashuhudia mchezo baina ya Minnesota Timberwolves waliyofanikia kufika hatua ya fainali baada ya miaka 20 kupita watawatembele Los Angeles Lakers ambayo itaongozwa na kinara wa magoli muda wote ndani ya NBA Lebron James ambaye atakuwa na msimu wake wa 22 ndani ya NBA
Ilhali Nyota Paul George akiwa na uzi wa Philadelphia 76ers atapambana na Milwaukee Bucks ya Giannis Antetokounmpo ambapo ni mchezo wa kukumbushia msimu 2023-24 ambapo 76ers walipoteza kwa alama 118-117 kwenye mchezo wa ufunguzi
LA Clippers wataanza makazi mapya kwenye dimba jipya la Intuit Dome mbele ya Phoenix Suns ilhali bingwa wa kanda ya Magharib Dallas Mavericks ambao ni wanafainili wa NBA 2023-24 chini ya Kyrie Irving na Luca Doncic watapambana na San Antonio Spurs ambayo imemuongeza nyota Klay Thompson kutoka Golden State Worriors
Huku Cris Paul atakayefikisha msimu wa 20 ndani ya NBA huku shughuli hiyo itamalizika kwa Mwamba Nikola Jokic akiwa na Denver Nuggets kupambana na Oklahama City Thunder chini ya Shai Gilgeous-Alexander
Kwenye mpangalio wa kalenda ya matukio,NBA wameendeleza utamaduni wa kipindi cha miaka 17 kwenye sikukuu ya X-Mass kuweka michezo ya Ligi ya Kikapu Marekani ambapo safari hiii kutakuwa na michezo 5 huku ikiwa ni makala ya 77 michezo ya NBA kuchezwa ndani ya X Mass ambapo inatumika kama sehemu ya zawadi kuelekea siku ya kufungua zawadi yaani Boxing Day mnamo Desemba 26-2024
Kumbukumbu tamu zaidi kwenye michezo ya NBA ndani ya X Mass ni Mlinzi wa Dallas Mavericks Luca Doncic kuweka rekodi ya kufunga alama 50,kutoa pasi za usaidizi mara 15 na kuchukua ribaundi mara 6,kupora mipira mara 4 na kuzuia mara 3 tangu msimu 1973-74
Kalenda ya matukio ya NBA imeendelea kutoa heshima, kukumbuka na kuenzi maisha ya Dr. Martin Luther King Jr. mnamo Januari 20 -2025 ambapo imeweka michezo mitatu maalumu kwa ajili ya kusherekea maisha yake kwa jamiii huku mbali na hilo NBA imeondoa michezo yote kwenye ratiba mnamo Novemba 05-2024 ambayo ni tarehe ya Uchaguzi nchini Marekani kutoa nafasi ya Wamerekani kufanya uchaguzi wa Rais nchini humo.
Unachopaswa kufahamu kuwa michezo 45 ndani ya Regural Sessiosn ndani ya NBA itaoneshwa ndani ya mabara ya Ulaya,Mashariki ya Kati na Afrika huku michezo na vipindi vya NBA vitaonekena kwenye nchi 214 duniani huku lugha 60 zitatumika kuzungumzia ligi ya mpira wa kikapu nchini Marekani ,
Je nani kushinda taji la NBA kwa msimu wa 2024-25?