Saturday , 17th Aug , 2024

 

Joe Biden amesema ana matumaini kwamba makubaliano ya kusitisha mapigano ya Gaza yanaweza kufikiwa.

"Tuko karibu zaidi kuliko tulivyowahi kuwa," rais wa Marekani alisema kufuatia duru ya hivi karibuni ya mazungumzo, akiongeza kuwa alikuwa akimtuma waziri wake wa mambo ya nje kwenda Israel kuendelea na "juhudi kubwa za kuhitimisha makubaliano haya".

Hata hivyo, afisa wa ngazi ya juu wa Hamas amesema kuwa hakuna maendeleo na wapatanishi walikuwa "wanauza udanganyifu".

Israel imesema "inathamini juhudi za Marekani na wapatanishi kuizuia Hamas kukataa kwake mkataba wa kuwaachia mateka".