Wednesday , 14th Aug , 2024

Afisa Mtendaji Mkuu wa Soko la Bidhaa Tanzania - TMX Godfrey Marekano ameeleza kuwa maandalizi ya uuzaji na uunuzi wa korosho msimu 2024/25 yameanza na yanaendelea vizuri.

Afisa Mtendaji Mkuu wa Soko la Bidhaa Tanzania - TMX Godfrey Marekano

Marekano amesema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Jijini Dar es Salaam, huku akiwataka wakulima wa korosho kuhakikisha kuwa wanazingatia ubora ili kuziongezea thamani sokoni.

"Tumekuwa na msimu mzuri katika mazao mengine kama Kahawa,Ufuta, Cocoa na sasa Mbaazi, lakini wakati huohuo tumeshaanza maandalizi kwa ajili ya uuzaji wa Korosho kwa mfumo wa kielektroniki,  naweza kusema maandalizi yanaenda vizuri " amesema Marekano.

Kuhusu utunzaji wa korosho ghafi, amewashauri wakulima kuhakikisha kuwa wanazingatia ubora pale watakapoanza mavuno ili kuendelea kuwavutia wanunuzi.