Friday , 9th Aug , 2024

Wafanyabiashara wa Soko la Shekilango wameiomba Serikali kuingilia kati suala la usafi wa Soko hilo kwani unakimbiza wateja na kuhatarisha usalama wa Afya za watumiaji.

Chemba za kuhifadhia maji taka soko la Shekilango.

Wameiambia EATV kuwa makaro ya kuhifadhia taka yamejaa na kutiririsha mpaka mitaani lakini uongozi wa Soko hilo haujajishughulisha kuuondoa.
"Soko letu linatumika na watu kutoka maneneo mbalimbali lakini sasa hivi wateja wanakimbia kwa sabau hawana pa kupit na mazingira ni mabaya sana uchfau ni mwingi hata sisi tunahofia kupata kipindupindu", David Andrew, Mfanyabiashara soko la Shekilango.

"Unaona hayo maji yanatoka kwenye zile chemba za maji naa damju wanapochinjia kuku yamekuja yametuhama hapa, sasa kama unavyoona hapo mpaka wengine wameunga maduka yao harufu ni kali lakini pia hatari kwa afya zetu", Filbert Kimambo, Mfanyabiashara soko la Shekilango.

"Unaona hapo mamalishe wanapika lakini maingira ni mabaya sana uchafu ni mwingi huwezi hata kunywa maji mtu umezungukwa na maji na chemba za maji taka ziko wazi zimejaa na uongozi wa soko haufanyi jitihada zozote haujali Afya zetu", Hawa Bororo, Mfanyabiashara soko la Shekilango.

Akiongea kwa niaba ya Mwenyekiti, mjumbe wa Soko hilo Said Athumani anasema wana utaratibu wa kuondoa taka mara tatu kwa siku, kwahiyo taka hizo ni kwa sababu hawafanyi usafi kila siku.
"Kwa mfano sasa hivi si unaona tumewakamata hawa wachinjaji kwa sababu ya mavazi yao , kwahiyo ni jambo ambalo huwa tunalifanya mara kwa mara na huo uchafu ni kwa sababu hapa usafi tutafanya tena jumamosi", Said Athuman, Mjumbe wa Soko la Shekilango.