Akizungumza leo Jijini Dar es Salaam,wakati wa hafla ya uzinduzi wa mitambo ya teknolojia ya Usaidizi wa Video kwa Waamuzi (VAR) itakayotumika ndani ya Ligi Kuu Tanzania Bara 2024-25,Amesema TFF inapaswa kupongezwa kwa maboresho na mikakati mizuri ya kuinua soka hapa nchini.
“soka la Tanzania limekuwa vizuri kwa sababu va maboresho vya miundombinu katika sekta zote ikiwemo Azam Media kuleta mitambo imara ambavo inaonesha soka letu kufika mbali”amesema Waziri Mkuu Kassim Majaliwa
Kwa upande mwingine,Naibu Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo Hamisi Mwinjuma na Rais wa TFF Wallace Karia wamesema matumizi ya teknolojia ya VAR itasaidia kuondoa malalamiko kutoka kwa wadau ya michezo hapa nchini.