Wednesday , 26th Jun , 2024

Rais wa Kenya William Ruto, amekataa kusaini Muswada wa Sheria ya Fedha ya mwaka 2024 ambao ulikuwa ukipingwa na Wakenya hali iliyopelekea vijana nchini humo wanaojiita 'Gen Z' kufanya maandamano.

Rais wa Kenya William Ruto

Kauli ya Rais Ruto ameitoa hii leo Juni 26, 2024, ikiwa ni siku moja tangu vijana nchini humo wafanye maandamano ambayo yalipelekea uharibifu mkubwa hasa katika eneo la Bunge nchini humo na kupelekea vifo na majeruhi.

"Sitosaini Muswada wa Sheria ya Fedha ya mwaka 2024 kutokana na shinikizo la umma," amesema Rais Ruto

Aidha Rais Ruto ameongeza kuwa, "Kwa sababu tumeuondosha Muswada wa Sheria ya Fedha wa mwaka 2024, inabidi tufanye mazungumzokama Taifa ya jinsi ambavyo tutaweza kuiendesha nchi pamoja na deni tulilonalo kwa pamoja, nitapanga kufanya mazungumzo na nitawasikiliza vijana wa nchi yetu na watoto wetu,".