Tuesday , 25th Jun , 2024

Mkuu wa wilaya ya Kisarawe Petro Magoti amepiga marufuku shughuli za ngoma kama vile mdundiko, unyago na sherehe za muziki na kuruhusu wanafunzi kujumuika na kuserebuka kwenye shughuli hizo na kumuagiza Mkuu wa Polisi wilaya vitendo hivyo vikibainika kufanyika akamate kuanzia mpiga ngoma,

Mkuu wa wilaya ya Kisarawe Petro Magoti

wazazi wa mtoto, aliyepewa tenda ya muziki hadi gari lililobeba muziki huo.

Akiongea  Wilayani Kisarawe wakati akikabidhiwa ofisi rasmi na Fatma Nyangassa, DC Magoti ametoa onyo pia kwa walimu wanaoanzisha mahusiano ya kimapenzi na wanafunzi wao kujiandaa kwani akiwabaini atawashughulikia 

"Nimesikia kuna walimu wanapenda wanafunzi sitaki kuwahukumu sijafika naendelea kupokea data zangu kama wewe unatafuna watoto wetu ambao Mh. Rais analeta pesa yule mtoto anakula anavaa anapendeza, yaani Mh. Rais anatoa matumizi wewe unakula!, serious?, halafu Mh. Rais anakulipa mshahara, umepewa nyumba ya serikali unaishi, umeme upo," amesema DC Magoti

Aidha akatoa maagizo kwa Afisa wa Maendeleo ya Jamii wilayani humo, "Kwahiyo andaa utaratibu wa semina na mikutano ya darasa la maadili kuanzia Julai mwaka huu kila shule tuwe na mambo ya maadili,  mtu yeyote anayetaka kuweka nguvu kuhusu unyanyasaji wa kijinsia twende nae, ukiona mtu ananyemelea kabinti kashule njoo niambie huyu alikuwa na mtoto nimemuona anamshika tutamshughulikia vibaya mno,"