Watoto wa marehemu pamoja na majirani waliokuwepo eneo la tukio wanadai kuwa walifika wanaume wawili wakiomba kuandikiwa barua ya kusafirisha mifugo,mwenyekiti huyo alipochukua karatasi na kalamu kutaka kuwaandikia barua ndipo walipoanza kumsambulia kwa mapanga mpaka kifo.
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Geita SACP Safia Jongo amethibitisha kutoka kwa tukio hilo huku chanzo cha tukio hilo kikiwa hakijafahamika na hakuna mtuhumiwa anayeshikiliwa mpaka hivi sasa.