Wednesday , 28th Feb , 2024

Msanii wa muziki wa Singeli Sholo Mwamba ametusanua kuhusu mpango wake wa kuachia albamu yake ya kwanza hivi karibuni ambayo ndani atamshirikisha Staa Diamond Platnumz, wawili hawa wote wanatokea Tandale.

 

Diamond Platnumz mwenyewe pia amethibitisha kuwepo ndani ya albamu hiyo kwa ku-share video ya Sholo Mwamba kwenye Insta Story yake na kuandika;

“MWAMBA THE ROCK, My homeboy brother, love always! Inshallah lazima niwepo kwenye album hiyo mwanangu!... ANOTHER BOY FROM TANDALE” – Diamond 

Jina la albamu hiyo ya Sholo Mwamba "ANOTHER BOY FROM TANDALE” linafuatia msukumo alioupata kutoka kwenye albamu ya tatu ya Mwana Tandale mwenzake, Diamond ya "A BOY FROM TANDALE," iliyotoka mapema mwaka 2018.