Tuesday , 20th Feb , 2024

Rapa na muimbaji wa Marekani Coi Leray ameibuka kusema kizazi chake hakijui jinsi gani ya kupika chakula.

Picha ya Coi Leray

Msanii huyo mwenye miaka 26 amefunguka hilo kupitia page yake ya mtandao wa X baada ya kuandika

“Sielewi kwanini kizazi chetu hakijui jinsi gani ya kupika, sitaki mpikie kwenye Air Fryer, Vuta sufuria hizo nzuri zilizokwaruzwa, washa r&B ya miaka ya 2000 na tuwachangamshe watu”.

Unakubaliana naye kuwa kizazi hicho cha miaka ya 90 hakijui kupika?