Wednesday , 14th Feb , 2024

Serikali wilayani Bukombe mkoani Geita inatarajia kuanza mchakato wa kuwachukulia hatua watumishi wa umma wanaopewa vyombo vya usafiri kwaajili ya kuwahudumia wananchi na badala yake vyombo hivyo kuvitumia kwenye shughuli zao binafsi jambo ambalo linasababisha vyombo hivyo kuharibika

Akizungumza wakati wa kukabidhi pikipiki tatu kwa Viongozi wa vyombo vya watumiaji maji Mkuu wa wilaya ya Bukombe Said Nkumba amewataka kuzitunza pikipiki hizo na kuhakikisha zinafanya kazi iliyokusudiwa na serikali.

“Usitumie pikipiki hizi tuu pikipiki hizi zinahitaji service bila service pikipiki hizi zitaharibika kwa muda mfupi sana mwende mkazingatie matumizi bora ya pikipiki hizi kwaajili ya kutoa huduma kwa wananchi wetu kwa sababu vyombo hivi ni vya serikali tutakuwa tunapita na kukagua kama kweli vinafanya kazi iliyokusudiwa” Said Nkumba, Mkuu wa wilaya ya Bukombe

“Kuna baadhi ya watumishi sio waaminifu ni wachache sio wote tutashirikiana na wananchi na viongozi wengine kuona pikipiki hizi zinafanya kazi iliyokusudiwa au zinafanya kazi tofauti kutokana na watumishi waliokabidhiwa vyombo hivyo” Bundala Maziku, Diwani kata ya Namonge

“Pikipiki hizi zimetolewa kuwasaidia kwenda kutembelea vyanzo vya maji wanakwenda kukusanya maduhuli ya serikali na kushughulikia changamoto mbalimbali ambazo zinajitokeza kwenye mradi husika na vyombo hivi vifanye shughuli ambayo imelengwa na sio vinginevyo” Mhandisi Jabir Kayila, Meneja wa RUWASA Mkoa wa Geita

Nao viongozi hao wameishukuru serikali kwa kuwatatulia changamoto ya usafiri kwani walilazimika kutumia gharama nyingi kwaajili ya usafiri jambo ambalo lilikuwa linawakwamisha kutoa huduma kwa wakati.

“Kutokana na changamoto tulizokuwa tunakutana nazo awali tulikuwa tunajikuta tunatumia hela za maji kukodi baiskeli kwasababu tulikuwa tunaenda umbali mrefu kuwafikia wateja kwakweli tunashukuru sana” Amos Robert, Mwenyekiti wa CBWSO Namonge

“Pikipiki hizi zitatusaidia sana kufanya kazi kwa ueledi sana na bila usumbufu na hapa tutajitahidi kutatua kero zote za wananchi kuusu maji kwa wakati” Masumbuko Stephano, Mwenyekiti wa CBWSO Katome

“Kwakweli usafiri haopo awali ulikuwa wa kudandia dandia lakini tunamshukuru mungu leo tumepata usafiri kwa sasa aina shida yoyote” Venance Katema, Mwenyekiti wa CBWSO Runzewe mashariki

Mpaka sasa RUWASA mkoa wa Geita wamefanikiwa kuchimba visima 22 ambapo kati ya hivyo visima 13 vimeanza kufanya kazi.

“Mpaka sasa ule mtambo wa kuchimba visima virefu umeshachimba visima 22 na visima 13 vimepata maji ya kutosha kusanifu miradi na kuwasambazia wananchi kwaiyo nitumie frusa hii kuwaasa na kuwaomba wananchi tuendelee kutunza vyanzo vya maji viendelee kutuhudumia” Jabir Kayila, Meneja wa RUWASA mkoa wa Geita.