Wakati Tanzania tunajivunia kuwa na ongezeko kubwa la watumiaji wa mtandao TikTok mpaka kufikia watu zaidi ya Milioni 1.6, Lakini hii ni maradufu kwa wenzetu nchini Marekani kwani takwimu za mwisho zinaonesha kuwa mtandao huo kwa nchini marekani unazaidi ya watumiaji milioni 150.
Nikurudishe nyuma kidogo, Mwaka 2022 nchini Marekani kupitia huyu huyu Joe Biden walipitishwa sheria za kukataza vifaa na mashirika ya serikali kutumia TikTok kwa sababu za kiusalama.
Lakini kuelekea uchaguzi mkuu mwaka huu nchini humo, tunamuona yule aliyekataza matumizi ya mtandao huo kwa watumishi wa serikali anajiunga na mtandao ule ule kwa lengo ya kurahisisha kampeni zake.
Inaweza kuwa na tafsiri tofauti kwa wachambuzi wa maswala ya siasa lakini kwa kuhitaji kuwafikia vijana kwenye hili ameshinda kwa sauti ya Manara ''Asubuhi''
Lakini kwa nchini Marekani ni kama vile Tanzania wale timu mgombea ''X'' siye tumezoea kuwaita chawa pia na kule wako, na ndiyo maana inasemwa kuwa mtandao huo utaendeshwa na ''team biden'' na si yeye.
Ni upi mtazamo wako kwenye hili?