Wednesday , 7th Feb , 2024

Klabu ya Yanga imezindua rasmi ofisi zake zilizopo maeneo ya Jangwani jijini Dar es Salaam mara baada ya kuzifanyai marekebisho.

 

Klabu ya Yanga imezindua rasmi ofisi zake zilizopo maeneo ya Jangwani jijini Dar es Salaam mara baada ya kuzifanyai marekebisho. Rais wa klabu hiyo Injinia Hersi Said amesema Sababu za kukarabati jengo hilo ni kuenzi mambo yaliyofanywa wazee wa Yanga miaka ya nyuma, pia ni kuhakikisha watendaji wa Yanga wanakuwa sehemu moja.

Injinia Hersi ameongeza kuwa Malengo yao Viongozi ni kufanya zaidi ya waliofanya wazee wa Yanga miaka 50 iliyopita.