Msuva alikuwepo katika kikosi cha Stars kilichoishia hatua ya makundi katika michuano ya AFCON 2023, nchini Ivory Coast.
Mshambuliaji huyo wa Kimataifa wa Tanzania, Simon Happygod Msuva amejiunga na klabu ya Al-Najma yenye maskani Mji wa Unaizah inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza nchini Saudi Arabia.
Msuva anajiunga na Al Najma kufuatia kuachana na JS Kabylie aliyojiunga nayo Agosti mwaka jana akitokea nyingine ya Ligi Daraja la Kwanza Saudi Arabia, Al-Qadsiah aliyoichezea kuanzia mwaka 2022.