
Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Geita ACP Amoni Mimata amesema tukio la mtoto huyo kuibiwa lilitokea Desemba 22,2023 saa tano usiku ambapo Swaumu alimvizia mama wa Mtoto huyo akiwa bafuni anaoga na akatumia nafasi hiyo kumchukua mtoto.
Kamanda Amoni amesema baada ya tukio hilo mama wa Mtoto huyo aitwaye Martha Philemoni alitoa taarifa Polisi na uchunguzi ukaanza na kufanikiwa kumkamata mtuhumiwa huyo.
"Baada ya kumkamata mtuhumiwa huyo akiwa na Mtoto, Mtoto tumemfanyia vipimo vyote vya afya na tumemkuta yuko vizuri bado jeshi tunaendelea na upelelezi ukikamilika mtuhumiwa tutampeleka mahakamani"