Thursday , 14th Dec , 2023

Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Ridhiwani Kikwete,amesema mfumo wa mahitaji ya rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma (HRA) hauna lengo la kumuondoa kazini ama kuwaonea watumishi wa umma hivyo hawana sababu ya kuuhofia mfumo huo.

Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Ridhiwani Kikwete

Kikwete amebainisha hayo wakati wa ufungaji wa mafunzo ya siku tatu kwa watumishi wa umma kutoka Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI) Shirika la Masoko Kariakoo na Bodi ya Sukari Tanzania yaliyofanyika MOI.

Amesema lengo la mfumo huo ni kuiwezesha kupima utendaji wa watumishi wake kwa njia rahisi na kuongeza ufanisi wenye tija kazini.

"Mfumo huu  hauna lengo la kukomoa watu, tutakuwa na utumishi wa umma unaotimiza majukumu, utawezesha kupanga utumishi wenye tija, huna sababu ya kuhofia," amesema Naibu Waziri Kikwete.

Amesema mifumo hiyo inakwenda kuonesha wapi kwenye mapungufu ili paweze kuboreshwa