Tuesday , 12th Dec , 2023

Director wa video za muziki Tanzania, Producer na msanii Nisher Bybee amefariki dunia usiku wa kuamkia leo saa 8:09.

Picha ya aliyekuwa Video Director Nisher

Kupitia ukurasa wa Geor Davie TV ambao unamilikiwa na baba yake mzazi Nabii Geor Davie umethibitisha taarifa ya kifo hicho na msiba upo nyumbani kwake Kisongo jijini Arusha.

Hizi ni baadhi ya video za nyimbo za BongoFleva ambazo ameziongoza Mama Yeyoo na Arosto za GNako Warawara, XO ya Joh Makini, Jikubali Ben Pol, Young Dee Kijukuu, Nje ya Box Nikki Wa Pili, Roma - 2030, Shilole - Nakomaa na Jiji, Jordan Ft. Mirror & Ngwea - Bila wewe, Fid Q Bongo Hip Hop na Killy Rudi.