Tuesday , 5th Dec , 2023

Mvua kubwa na upepo mkali unalikumba jimbo la kusini mwa India la Andhra Pradesh wakati kimbunga kikali kikipiga nchi kavu. Watu tisa, ikiwa ni pamoja na mtoto, wamefariki katika jimbo la Andhra Pradesh na jimbo jirani la Tamil Nadu katika matukio yanayohusiana na mvua.

 Mamlaka zimewahamisha maelfu ya watu kutoka maeneo ya chini katika majimbo yote mawili.

Maeneo mengi ya makazi yamefurika, na video zinaonyesha magari yakielea katika maji.Kimbunga Michaung kimesababisha maporomoko ya ardhi.

 Idara ya Hali ya Hewa ya India (IMD) imesema kuwa kimbunga hicho kitakuwa na kasi ya upepo hadi kilomita 110 kwa saa ,ambacho kitapungua wakati kimbunga hicho kikiendelea kuvuma baada ya kuanguka kwa ardhi.

Takriban watu 9,500 katika jimbo la Andhra Pradesh wamehamishwa hadi katika kambi 211 za kutoa misaada.

Mtoto wa miaka minne alifariki   baada ya ukuta kuanguka, vyombo vya habari nchini humo vimemnukuu afisa wa serikali akisema.

Vifo vinane viliripotiwa katika jimbo la Tamil Nadu, ambako kimbunga hicho kilisababisha uharibifu siku ya Jumanne  sababu zilizojumuisha kuanguka kwa miundo na umeme.

Maafisa wa hali ya hewa wametoa tahadhari nyekundu katika baadhi ya maeneo ya majimbo ya Tamil Nadu na Andhra Pradesh. Shule, vyuo na ofisi nyingi zimefungwa katika wilaya kadhaa.