Saturday , 2nd Dec , 2023

Mashambulizi mapya ya Israel katika Ukanda wa Gaza yanaendelea katika siku yake ya pili, wakati jeshi likiwaonya raia katika baadhi ya maeneo kuondoka

Malori ya misaada yameruhusiwa kuingia Gaza kutoka Misri kwa mara ya kwanza tangu kumalizika kwa mapigano siku ya Ijumaa.

Malori ya misaada yameruhusiwa kuingia Gaza kutoka Misri kwa mara ya kwanza tangu kusitishwa kwa mapigano Ijumaa

Israel inasema imeiondoa timu yake ya mazungumzo kutoka Qatar, ambayo ilikuwa ikipatanisha mazungumzo juu ya kusitisha mapigano zaidi.

Wizara ya afya ya Hamas katika Ukanda wa Gaza imesema zaidi ya watu 193 wameuawa tangu mashambulizi hayo yaanze tena. Jeshi la Israel lasema limeshambulia maeneo 400 katika ukanda huo

Vingóra vya tahadhari pia vilisikika katika baadhi ya maeneo ya Israel siku ya Ijumaa, huku roketi zikirushwa kutoka Gaza zikizuiwa.

Shambulio la Hamas dhidi ya Israel Oktoba 7 liliuwa watu 1,200, huku wengine 240 wakitekwa nyara.

Tangu wakati huo, wizara ya afya ya Gaza inayoongozwa na Hamas inasema zaidi ya watu 14,800 wameuawa katika kampeni ya kulipiza kisasi ya Israel, ikiwa ni pamoja na watoto 6,000.