Wednesday , 29th Nov , 2023

Droo ya mashindano ya kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) imepangwa leo Novemba 29, 2023 ambapo Vigogo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Simba, Yanga na Azam wamepewa vibonde katika hatua ya kusaka tiketi ya 32 bora.

Katika droo hiyo iliyoshirikisha jumla ya timu 64, Mabingwa watetezi Yanga SC wamepangwa dhidi ya Haulung ya daraja la kwanza wakati Simba wakiwakaribisha Tembo FC ambao ni Mabingwa wa Ligi ya Mkoa wa Tabora huku Azam wakiwa wenyeji wa Alliance kutoka Mwanza.

 

Mechi hizi zitaanza kuchezwa kuanzia Desemba 15 hadi 17, 2023.