Baada ya mchezo wa Ligi ya mabingwa Afrika dhidi ya Asec Mimosas ambao ulimalizika kwa sare ya bao 1-1 moja ya shabiki wa Simba alisikika akihoji kwa nini viongozi hawatuambii ni changamoto gani ambazo tunapitia mpaka timu kufanya vibaya.
“Watu wamegoma kuja uwanjani, timu wamemsusia Ahmed Ally. Ahmed Ally ndo anazunguka kuwarudisha mashabiki uwanjani, kweli viongozi tunao? viongozi wote wamekaa kimya kwa nini wasijitokeze waseme changamoto tunazopitia ni 1,2,3,4 wamemuachia Ahmed Ally, sawa sisi tumemsikiliza Ahmed Ally tumekuja uwanjani ndo tupate mateso haya uwanjani. Watakuja wenyewe uwanjani.” Amesema shabiki wa Simba SC
Sare dhidi ya Asec ilikuwa sare ya 6 msimu huu Simba wanapata Kwenye michezo 13 waliyocheza. Wametoka sare kwenye michezo 3 ya Ligi ya mabingwa, wana sare 2 kwenye michuano ya African Footbaal League na sare 1 kwenye Ligi Kuu na wamefungwa mchezo 1 tu.