Sunday , 26th Nov , 2023

Miaka 12 imepita tangu macho ya mashabiki na wapenzi wa klabu ya Manchester United yalipobarikiwa kuona moja kati ya goli bora kuwahi kufungwa

 

Na aliyewahi kuwa kiungo wa timu hiyo Wayne Rooney February 12, 2011 kwenye mchezo dhidi ya majirani zao Manchester City.

Baada ya mchezo ule mwandishi mmoja kutoka ''Sky sports'' alimuuliza Wayne Rooney ''Have you scored an over head bicycle kick before?''

Kwa sauti ya kicheko Wayne Rooney alimjibu kwa kusema kipindi niko shule, lakini nadhani ni la kwanza nikiwa kama mchezaji wa kulipwa.

Tarehe 26/11 miaka 12 baadaye, inakuja kushuhudiwa ''bicycle kick'' kutoka kwa kijana mchanga kabisa kwenye klabu ya Manchester United Alejandro Garnacho, goli ambalo baadhi ya mashabiki wa mpira wanalitaja na kulitabiria ya kuwa huwenda likawa goli bora la msimu.

Kwa aina hiyo ya ufungaji wa magoli ya ''bicycle kick'' ndiyo maana ya swali hilo lililouliza kuhusu utofauti wa Wayne Rooney na Alejandro Garnacho ni nini?

Picha: Skysports