Thursday , 23rd Nov , 2023

Mfalme wa muziki wa Afrobeats Davido amepewa siku ya heshima "Davido Day" kila itakapofika siku ya Novemba 18, pia amepewa siku ya heshima nyingine ya kumthamini Novemba 21 katika mji wa Atlanta nchini Marekani.

Picha ya Davido

Heshima hiyo amepewa na Meya wa 61 wa Atlanta "Andre Dickens" pamoja na Bodi ya Baraza la Fulton, Georgia kwa kutambua mchango wake katika kiwanda cha burudani.

Hii ni baada ya staa ya huyo kutoka Nigeria #Davido kufanya Tamasha kubwa la Burudani na kuuza tiketi huko Atlanta katika ukumbi wa State Farm Arena.