Saturday , 15th Mar , 2014

26 wajitokeza michuano ya wazi ya chess Tanzania

Chama cha mchezo wa chess Tanzania TCA hii leo kimeendesha mashindano ya wazi ya siku mbili yakihusisha wachezaji toka vilabu mbalimbali hapa nchini mashindano yanayofanyika katika ukumbi wa Gymkhana klabu jijini Dar es salaam

Mwenyekiti wa TCA Geofrey Mwanyika amesema kuwa tangu uongozi wao mpya umeanzisha mashindano hayo ambayo hufanyika mara moja kwa kila mwezi mwitikio kwa mwezi huu wa pili umekua mkubwa ukilinganisha na miezi miwili iliyopita
Mwanyika amesema kuwa mwezi huu idadi ya washiriki imefikia 26 huku ikiendelea kuongezeka tofauti na mwezi uliopita ambako walishiriki wachezaji 15 pekee

Naye mmoja wa wachezaji nguli wa mchezo huo Yusuf Mdoe amesema kuwa ushindani katika chess miaka ya nyuma ulikua mkubwa sasna tofauti na miaka hii lakini pia akatoa pongezi kwa uongozi mpya wa TCA kwa juhudi kubwa wanazozifanya ili kurejesha hadhi ya mchezo huo na anamatumaini mkakati wa kupeleka mchezo huo mashuleni utasaidia