Pengine ulishwahi kusikia nyingi ambazo zilimzungumzia mwanaume na mengi anayopitia kwenye maisha, kwa mujibu wa wavuti wa worldmeter unasema kwa wastani maisha ya mwanaume ni miaka 70.8.
Tarehe 14, April mwaka huu, mwanamuziki kutokea nchini Canada mwenye asili ya Nigeria Dax aliachia wimbo wake ulipewa jina la ''To be a Man'' anachojaribu kueleza humu ndani ni changamoto anazopitia mwanaume kwenye maisha na kushindwa kuheshimika mpaka pale atapofanikiwa kuweka msosi mezani.
''And they don't care 'bout what you know
It's not 'bout how you feel
But what you provide inside that home''
Ukiachana na Dax, Nakurudisha tena Tanzania, Kwa mwanamuziki Nicas John Marwa kwenye NIDA; ila kwa kuokoa nguvu na muda muite Nikki Mbishi.
Chini ya M-Lab kutoka palipo sikika sauti ya gari yenye mwendo ''Tongwe Record'' ilitengenezwa Albamu ya kwanza ya Nikki mbishi iliyofahamika kama ''Sauti ya Jogoo''
Wimbo namba 13 uliyopewa jina ''Nimezama'' anasema - ''Punde nikaanza kazi ya kubeba mizigo, Mabox pandisha ngazi sita sita kwa mpigo, tenda ngumu eenh! bhana duh!, -
ngoja nijikomaze flow 9 kwenda juu, nadhiki ngoja nijikaze, alimanusura nijute kuzaliwa mtoto wa kiume, usiombe yakukute mwanangu mswalie mtume''.
Kutokana nayote ambayo umekwisha pitia kwenye maisha hadi sasa, Umeshawahi kujuta kuzaliwa mwanaume.
NB: Hii ni sanaa tu hakuna dhamira nyingine yeyote juu ya andiko hili,