Thursday , 16th Nov , 2023

Mdau wetu wa SUPATECH aliomba tumfahamishe namna ambavyo ataweza kufungua YouTube channel yake. 

Nasi bila hiyana tunakaona siyo mbaya elimu hii tukaiweka wazi na huwenda ikawa faida kwa wadau wengi wa SUPATECH

 

Hizi hapa ni baadhi ya hatua ambazo unaweza kuzifuata ili kukamilisha kufungua YouTube channel ya kwako

Ikiwa kama tayari una-akaunti ya google fuata hatua hizi.

1. Ingia kwenye YouTube YouTube.com  alafu nenda upande wa kulia palipoandikwa sign-in , alafu weka e-mail yako ambayo ungependa kuitumia kwenye YouTube akaunti yako.

2. Baada ya kuingiza E-mail yako, nenda upande wa kulia juu ambapo kuna herufi ya jina lako/Picha yako. Inategemeana kama kwenye G-mail akaunti uliweka picha au hukuweka.

Ukishaenda, bonyesha ile picha au herufi husika. alafu chagua neno la kwanza lililoandikwa ''creat a channel''

3. Tengeneza akaunti yako, hapa utapewa machaguo mawili moja ni kutengeneza kwa kutumia jina na profile picture yako na nyingine ni ya kutengeneza kutegemeana na nini unahitaji ikiwa kama jina la kampuni/biashara husika. hivyo utaweka picha na jina ambalo litakuwa tofauti na jina la akaunti yako.

Baada ya kukamilisha kutengeneza akaunti yako ya YouTube baadhi ya vitu vingine vinafuata, kwenye kutengeneza muonekano wa akaunti yako. Ili mtazamaji atakapoingia kwenye channel yako aweze kufahamu na kutambua kwa urahisi, vitu hivyo ni kama vile;

a). Ni kuweka ''Profile picture'' ambayo itakaa kama sehemu ya utambulisho wako mkubwa kama sisi ambavyo unaona namba tano.

b). Ongeza maelezo kidogo kuhusu channel yako.

c). Ongeza viambatanisho vingine (links) kuhusu mitandao yako mingine ya kijamii, kama vile instagram, facebook na X 

Hongera umefanikiwa kukamilisha zoezi la kutengeneza YouTube channel yako.

Picha: @Buffer