Thursday , 9th Nov , 2023

Rapa Roma Zimbabwe amefunguka kuchukizwa na kauli ya Wakazi kumwambia kwamba alijiteka mwaka 2017 ili kuonewa huruma na mashabiki na kuongeza wafuasi wa muziki.

Picha ya Roma Mkatoliki

"Haya ndio mambo yanayomfanya yule Rapper aliyekosa Ubunge Ukonga kwa kupata kura Asilimia 1.4! Sikia Wewe Bwana Mdogo @wakazi huna nidhamu na waliokutangulia kwenye huu mchezo basi Muheshimu hata dada yetu".

"Punguza Nyenyenye na ukiendelea napost Video zako za show Mwanza raia wakikurushia makopo wakikwambia Shukaaaa, Shukaaaaa!! tunakustiri tu. Umenikera sana kunambia nilijiteka". ameandika Roma

Roma ameshea hilo baada ya kujibizana kwa maneno kati yake na Wakazi kupitia mtandao wa X.