Wednesday , 8th Nov , 2023

Nyota wa ligi ya NBA anayekipiga katika klabu ya Timberwolves, Anthony Edwards aisaidia timu yake kuvuruga spidi waliyoanza nayo klabu ya Celtics kwenye ligi ya msimu huu kwa kucheza michezo mitano mfululizo bila kupoteza.

Nyota Anthony Edwards alikuwa mwiba mchungu kwa Boston baada ya kuwabababua vilivyo kwa kufunga alama 38, rebounds 8 na assists 7 huku akimzuia kwa ustadi mkubwa nyota Jayson Tatum asiweze kuleta madhara dhidi yao.