
Askari wanawake
Hayo yameelezwa jijini Dar es Salaam katika maadhimisho ya 23 ya azimio la 13-25 ambalo linalenga kuwashirikisha askari wanawake katika misheni za ulinzi wa amani yaliyofanyika katika Chuo cha Taifa cha Ulinzi Tanzania Kunduchi jijini Dar es Salaam.
Kamishina wa Utawala na Rasilimali watu wa Jeshi la Polisi CP Suzan Kaganda, amesema changamoto kubwa iliyokuwepo siku za nyuma kwa askari wanawake ni uthubutu na utayari wa ushiriki katika ulinzi wa amani ambapo amebainisha kuwa kwa sasa askari wanawake wamekuwa wakishiriki misheni za ulinzi wa amani kutoka na elimu na kupata kipaumbele na mafunzo ya ulinzi wa amani.
Mwakilishi wa UN women Tanzani Hodan Addou, amesema lengo la Umoja wa Mataifa ni kuwashirikisha askari wanawake katika misheni za ulinzi wa amani ambapo amebainisha kuwa katika misheni za ulinzi wa amani kumekuwepo na changamoto kubwa kwa makundi ya wanawake na watoto.
Ameeleza kuwa wahanga wakubwa katika machafuko ya kiusalama yanapotokea ni wanawake na watoto huku akisema umoja wa mataifa utaendelea kuweka mazingira bora ya kiusalama kwa makundi hayo.
Kwa upande wa uongozi wa kituo cha mafunzo ya ulinzi wa amani umesema umeongeza nafasi za udahili kwa askari wanawake katika mafunzo ili kuongeza uwakirishi wao katika misheni mbalimbali za umoja wa mataifa.