
Mafuta
Tanga, Petroli ni Tsh. 3,274 kutoka Tsh. 3,327, Dizeli imepanda kutoka Tsh. 3,494 hadi Tsh. 3,510, Mafuta ya Taa yamepanda hadi Tsh. 3,469 kutoka Tsh. 2,989. Mtwara, Petroli itauzwa Tsh. 3,347, Dizeli Tsh. 3,546 na Mafuta ya Taa yamepanda hadi Tsh. 3,495 kutoka Tsh. 3,016.
Kutokana na tangazo hilo la bei hizo mpya, inaonyeshakuwa petroli imeshuka kwa Sh7 kwa lita wakati dizeli imeshuka kwa Sh74 kwa lita, huku mafuta ya taa yakipanda kwa Sh480 kwa lita, tofauti na bei ya kikomo zilizotangazwa mwezi uliopita kwa mkoa wa Dar es Salaam.
Kwa upande wa Tanga, petroli itauzwa kwa Sh3,274 kutoka Sh3,327, huku dizeli ikiwa imepanda kutoka Sh3,494 hadi Sh3,510; na mafuta ya taa yatauzwa Sh3,469 tofauti na ilivyokuwa mwezi uliopita ambapo yaliuzwa Sh2,989.
"Mabadiliko ya bei za mafuta kwa mwezi Oktoba 2023 yanatokana na kupungua kwa bei za mafuta katika soko la dunia kwa wastani wa asilimia 5.68 na gharama za uagizaji wa mafuta kwa wastani wa asilimia 13 kwa petroli," imeeleza taaria hiyo