Thursday , 26th Oct , 2023

Takriban watu 16 wanahofiwa kuuawa katika shambulio la risasi katika mji wa Lewiston mjini Maine nchini Marekani.

Mshukiwa huyo bado yuko huru .

Walisema kuwa anapaswa kuchukuliwa kuwa "mwenye silaha na hatari" na amewaambia wakazi wa Lewiston na Lisbon ya karibu wajihifadhi.

Polisi wamemtaja Robert Card, mwenye umri wa miaka 40, kama mshukiwa mkuu, wakisema kuwa "ana silaha na hatari".

Mtu huyo mwenye silaha bado yuko huku  mamia ya maafisa katika jimbo hilo wanahusika katika msako huo.Mama mmoja ambaye alikuwa na familia yake wakati wa shambulio hilo, anasema alimlaza binti yake, 11, ili kumlinda.

Lewiston, mji mdogo wa karibu 38,000, umewekwa kwenye  karantini huku  biashara zimeambiwa kufungwa na watu kukaa nyumbani.