Wednesday , 25th Oct , 2023

Muungano wa Walimu wa Elimu ya Msingi nchini Kenya (KUPPET) umeitaka serikali kutoa mafunzo ya kijeshi kwa walimu wanaofanya kazi katika maeneo yasiyo salama kote nchini na kuwapa bunduki ili kuimarisha usalama wao

Wakizungumza mjini Isiolo wakati wa mkutano mkuu wa mwaka huu, maafisa wa KUPPET  na walimu kutoka kaunti ya Isiolo wanasema kuwa walimu wanaendelea kuhangaishwa na kutishwa na Tume ya Utumishi wa Walimu kuendelea kufanya kazi katika mazingira hatarishi

Edward Obwocha ambaye ni Katibu wa Taifa wa chama hicho amewataka walimu hao kutoa wito wa kutolewa kwa bunduki na walimu walikubaliana kwa pamoja 

Hivi karibuni ya Tume ya Utumishi wa Walimu aliwashtaki  walimu waliotoroka kutoka maeneo ya Kaskazini mwa Kenya ambako maisha yao yalikuwa hatarini ambapo walimu hao wanasema ni kinyume na utaratibu kwa kuwa walikimbia ili kulinda maisha yao