Friday , 20th Oct , 2023

Shirika la Umoja wa Mataifa la wakimbizi wa Kipalestina linasema kwamba Gaza sasa ni "janga" kwa raia na muda unakimbia kwa ajili ya kupata misaada katika eneo hilo. 

 

 Mashirika ya kutoa misaada yanatumai malori 20 ya misaada yataingia leo lakini yanasema mengi zaidi yanahitajika.

Gaza bado inazingirwa na Israel kuzuia usambazaji wa maji, umeme, chakula na mafuta katika mpaka wake.

Waziri mkuu wa Uingereza Rishi Sunak anahudhuria mazungumzo nchini Misri huku hofu ikiongezeka kwamba mzozo huo unaweza kusambaa

Maafisa wa Palestina wanasema zaidi ya watu 3,700 wameuawa katika Ukanda wa Gaza tangu Hamas ilipoishambulia Israel Oktoba 7 na kuua zaidi ya watu 1,400.

Siku ya Alhamisi, kanisa la kikristo la Orthodox katika mji wa Gaza ambapo maafisa wa kanisa wanasema mamia ya watu walikuwa wakihifadhi walishambuliwa

Israel inasema kuwa ndege zake zililenga kambi ya karibu ya Hamas iliyokuwa ikitumiwa kurusha roketi katika eneo lake na ilikuwa ikichunguza tukio hilo.

Ofisi ya habari ya serikali ya Gaza imesema watu 18 wameuawa; Kanisa halikutangaza idadi ya vifo.