
Matokeo ya awali kutoka asilimia 99.9 ya vituo 5,890 vya kupigia kura nchini humo yanaonyesha kuwa hakuna hata mmoja kati ya wagombea wawili wanaoongoza aliyepata zaidi ya asilimia 50 ya kura zilizotangazwa mshindi.
Bw Weah kwa sasa ana asilimia 43.8 ya kura huku Bw Boakai akiwa na asilimia 43.5, kufuatia uchaguzi wa Oktoba 10, matokeo ya muda yanaonesha.
Tume ya Taifa ya Uchaguzi bado haijatangaza duru ya pili.Katika mkutano na waandishi wa habari siku ya Alhamisi, Bw Boakai aliwataka wagombea wenzake wa upinzani kujiunga na "timu ya uokoaji kwa ushindi wa kishindo".
Aliongeza kuwa "Tunawafikia ndugu zetu wa upinzani na Waberia kwa ujumla kuungana nasi katika kazi hii tukufu ya kuifanya nchi yetu ipumue kwa uhuru tena," .
Hakuna hata mmoja kati ya wagombea wengine 18 aliyepata zaidi ya asilimia 3 ya kura.Duru ya pili inatarajiwa kufanyika Novemba 7 baada ya kutangazwa kwa matokeo rasmi.
Boakai, ambaye alihudumu kama makamu wa rais katika serikali ya aliyekuwa rais wa wakati huo Ellen Johnson, aliendesha kampeni yake chini ya kauli mbiu ya "Rescue".
Bw Weah anasema serikali yake ilipiga hatua kubwa katika muhula wake wa kwanza, ikiwa ni pamoja na kuanzisha masomo ya bure kwa wanafunzi wa vyuo vikuu.