Thursday , 19th Oct , 2023

Kaimu Msajili wa Vyama vya Michezo wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Wakili Evordy Kyando amesimamisha Uchaguzi wa Chama cha Mpira wa Miguu Temeke (TEFA) uliokuwa ufanyika Oktoba 22, 2022 hadi hapo atakapotoa maelekezo mengine.

Uchanguzi huo ulitakiwa kufanyika kuziba nafasi ya Mwenyekiti wa Chama hicho Peter Mhinzi aliyefariki 2022 na kutakiwa kupatikana kwa mtu mwingine kwa mujibu wa Katiba.

Akieleza hayo Oktoba 19, 2023 Msajili Kyando  alisema alipokea barua kutoka wa Wanachama wa TEFA wakidai kuwa wanaingiliwa katika mchakato wao wa kufanga uchanguzi na mamlaka ya juu ya Soka ikiwemo Chama cha Mkoa (DRFA) na Shirikisho la mpira wa Miguu Tanzania (TFF).

Baada ya kupokea malalamiko ya Wanachama hao, BMT walifanikiwa kuzungumza mamlaka zote tatu ikiwemo TEFA, DRFA na TFF kila mmoja kwa wakati wake.

“Kwa kuwa muda ulikuwa mdogo kupitia vielelezo vya pande zote mbili, tunaona tuchukue uamuzi mdogo wa uchanguzi huu kutofanyika kwa siku hiyo ya jumapili hadi hapo tutakapopitia kwa uyakinifu vielelezo vyote.

Tunahitaji kila mmoja kupata haki zake katika hili, tumeona kwanza tufanye maamuzi hayo madogo hadi hapo tutakapomaliza mchakato wa kupitia vielelezo vya pande zote ikiwemo TEFA,  DRFA na TFF.