
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, wakati wa mahafali
Akiongea kabla ya kuhitimisha duru la pili la mahafali ya 53 ya chuo hicho, Dkt. Kikwete amesema kwamba kafurahishwa na kuona wanawake siku hizi wakiupiga mwingi na kuwataka vijana wa kiume walichukulie jambo hilo kama changamoto kwa wao kufanya vizuri zaidi kwenye masomo.
Katika mahafali hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa Mlimani City, jumla ya wahitimu 2796 walihudhurishwa ambapo 2700 walitunukiwa shahada za awali ikiwa ni wasichana 1488 na wavulana 1212.
Jumla ya Stashahada 78 zilitolewa kwa wanaume 45 na wasichana 33, wakati wanaume 10 na wasichana wanane walitunukiwa Astashahada.