Thursday , 28th Sep , 2023

Taharuki imetokea kwa wakazi wa mtaa wa Azimio Kata ya Igogo jijini Mwanza, baada ya moto umbao haujafahamika chanzo chake kuteketeza gari ndogo aina ya Toyota Crown.

Gari iliyowaka moto

Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo wamesema baadhi ya watu walinusurika kuungua na moto huo baada ya kujaribu kusogea eneo la tukio wakati moto ukiwaka kwa nguvu.

Jeshi la zimamoto mkoa wa Mwanza limefika na kufanikiwa kuuzima moto huo.

Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia leo Septemba 28, 2023, na baada ya kuungua mwenye gari aliondoka na kuahidi atarejea ambapo hadi sasa bado hajarudi.